Loading...

MTOTO WA MAAJABU MWENYE MIGUU MINNE NA JINSIA MBILI AZALIWA - NIGERIA

Loading...
Baada ya binti kuzaa mtoto mwenye miguu mitatu huko Kaduna, Nigeria, mke wa pili wa mtu aliyejulikana kwa jina la Malam Hassan Ibrahim, amejifungua mtoto mwenye miguu minne na jinsia mbili huko Magama JIbya, Jimbo la Katsina.

Kwa mujibu wa mtandao wa Dailytrust, Zainab (20) alijifungua mtoto huyo Machi 9, 2018. Hassan na Zainab walioana miaka minne iliyopita na walibarikiwa kupata mtoto wa miaka mitatu wa kiume, Fahad.

Akimuelezea mtoto, Hassan alisema, "Mtoto anajinsia mbili na miguu minne, miguu miwili isiyo ya kawaida na uume vipo pembeni ya ubavu wake wa kushoto, ni mguu mmoja kati ya miwili iliyoongezeka ndio unafanya kazi. Ninaweza kusema ni msichana kwa sababu miguu mirefu na ya kawaida ina jinsia ya kike katika mahali sahihi."
Na Geofrey Okechi - Dar es salaam.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za gossip punde zinapojiri.
MTOTO WA MAAJABU MWENYE MIGUU MINNE NA JINSIA MBILI AZALIWA - NIGERIA MTOTO WA MAAJABU MWENYE MIGUU MINNE NA JINSIA MBILI AZALIWA - NIGERIA Reviewed by By News Reporter on 3/17/2018 11:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.