Loading...

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WAGOMA KISA NYAMA YA KUKU - UGANDA

Loading...
Imezoeleka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kufanya migomo kwa sababu zisizo na tija lakini katika Chuo Kikuu hiki kilichopo Ntebe, wanafunzi wameonekana kugomea chakula kwa kukosa kuwekewa nyama ya kuku katika chakula.

Kutokana kutogewa kuku kwa muda wa siku tatu ikiwa kama sababu kuu, wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nkumba nchini Uganda waliamua kugoma ili kuwahimiza uongozi wa taasisi hiyo kurekebisha chakula chao.

Kwa mujibu wa kauli iliyotolewa na katibu mkuu wa chuo, alisema wanafunzi wamegomea masomo kwa sababu hawakuwekewa kuku katika chakula chao.

Walienda mbali zaidi kwa kulalamikia maswala mengine kama kuwekewa kiasi kidogo cha chakula, ubora mdogo wa nyama, kukosekana kwa vikombe vya kunywea maji, na maziwa kutokuwepo.

Ijapokuwa, Utawala ulionekana kuwasikiliza malalamiko yao yaliyowasilishwa na wanafunzi na walitoa kauli ya kuwaomba kuwa wakarimu na wasikivu kwa kuwa wanashughulikia tatizo lao.
Na Hamis Shakhi - Entebe, Uganda.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za gossip punde zinapojiri.
WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WAGOMA KISA NYAMA YA KUKU - UGANDA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WAGOMA KISA NYAMA YA KUKU - UGANDA Reviewed by By News Reporter on 3/17/2018 10:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.