Loading...

ZANZIBAR: WAZIRI AAGIZA KUPELEKWA WATAALAM HOSPITALI YA ABDALLA MZEE

Loading...
WAZIRI wa Hamad Rashid Mohammed, ametoa agizo kwa katibu mkuu na ofisa mdhamini  wa wizara hiyo Pemba, kuhakikisha katika kipindi cha mwezi mmoja katika hospitali ya Abdalla Mzee inakuwa na wataalamu wa kutoa huduma stahiki na kwa wakati.

Alisema   hakuna sababu ya kuwa na hospitali yenye mashine na vifaa vya kila aina huku vikishindwa kutumika kwa sababu ya kukosa wataalamu wa kutumia vifaa na hivyo wananchi kushindwa kupata huduma za kiafya.

Aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na watendaji wa hospitali hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kisiwani Pemba, kutembelea taasisi zilizochini ya wizara yake.

“Hatuwezi kumnyima mgonjwa huduma kwa ajili ya kukosa wataalamu wala hatushindwi kuwambia wachina watuengeze wataalamu kama waliweza kutusaidia mengine tunawezaje kuwaomba hili, lazima tulisimamie hili wataalamu wapatikane”,alisema.

Aidha aliagiza kila hospitali kuekwa visanduku vya maoni hali ambayo itasaidia wananchi kuweza kutoa malalamiko yao ili kujua changamoto zinazowakabili wananchi kila baada ya siku 15 za mwezi na kuweza kufika kwake na baada ya siku tatu kupatikana majibu ya malalamiko hayo.

“Kila tulipotembelea hatukuweza kupata malalamiko yoyote kwa wagonjwa, dawa pia tumeambiwa zipo lakini pia tumeona usafi ni mzuri upo wa kutosha tuendelee kufanya bidii zaidi kudumisha haya”, alisema.

Hata hivyo Waziri huyo, aliwataka madaktari hao kushirikiana katika utendaji wa kazi zao ili kuweza kuzitumia taaluma zao kama inavotakiwa.

Nae Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Haji Mwita Haji, alisema  katika hospitali yao kuna uhaba wa madaktari ikiwemo wahudumu ambapo huifanya hospitali yao kukosa kuwashuhulikia wagonjwa kwa muda.

“Kuna baadhi ya muda wagonjwa ni wengi hivyo maodali ni wachahe hali ambayo inatupa usumbufu kwetu, lakini pia madaktari ambao hupewa uhamisho kuja Pemba hawafiki wanafikia kuenda masomoni ni changamoto kubwa kwetu” , alisema.

Naye ofisa Mdhamini wa wizara ya Afya Pemba, Shadya Shaban, alisema lengo la serikali ni kuifanya hospitali ya Abdalla Mzee kuwa ni ya Mkoa, hivyo ni vyema kuona inatoa huduma katika muda muafaka kwa wagonjwa.
Na Geofrey Okechi.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
ZANZIBAR: WAZIRI AAGIZA KUPELEKWA WATAALAM HOSPITALI YA ABDALLA MZEE ZANZIBAR: WAZIRI AAGIZA KUPELEKWA WATAALAM HOSPITALI YA ABDALLA MZEE Reviewed by By News Reporter on 3/17/2018 09:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.