Loading...

MWANAFUNZI AMPA UJAUZITO MWALIMU WAKE

Loading...
Wakati ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.

Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.

Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.

Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku 'mzazi' huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.

Baadhi ya wazazi mkoani hapa wamekuwa na maoni tofauti na wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia 'kujiachia' kimapenzi kwa mwanafunzi wake.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
MWANAFUNZI AMPA UJAUZITO MWALIMU WAKE MWANAFUNZI AMPA UJAUZITO MWALIMU WAKE Reviewed by By News Reporter on 3/12/2018 07:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.