Loading...

NINAAMINI KILA BINADAMU ALIKUSUDIWA MAFANIKIO - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Ninaamini kila binadamu alikusudiwa MAFANIKIO na kuwekewa ndani yake MBEGU ya kutenda mambo makubwa katika dunia hii. Hii inamaanisha hata WEWE ni mmoja wao. Wewe ni mtu muhimu sana katika dunia hii na una UWEZO mkubwa sana ndani yako wa kufanya mambo makubwa.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa ukawa umeambiwa na watu mbalimbali kwamba UWEZO wako ni mdogo na wewe ukachagua KUAMINI maneno yao. Ukaambiwa wewe hutafanikiwa nawe ukakubali na kuamini. Inawezekana watu hawakuamini nawe ukapoteza kujiamini kuwa unaweza

Jambo moja naomba nikueleze, una UWEZO mkubwa ndani yako, kuna MBEGU ya mafanikio ndani yako ambayo inakusubiri uimwagilie maji iweze KUCHANUA na KUSTAWI. Usiamini kuambiwa huwezi, UNAWEZA, tumia uwezo ulionao.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen

Tuma neno 'MAKALA' kwenda +255765112259 kupata mwendelezo wa siri za utajiri punde zinapojiri.
NINAAMINI KILA BINADAMU ALIKUSUDIWA MAFANIKIO - Na Siri ya Utajiri NINAAMINI KILA BINADAMU ALIKUSUDIWA MAFANIKIO - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 3/12/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.