Loading...

ORODHA YA WANAMUZIKI WA HIP HOP MATAJIRI 2018 - JAY Z AONGOZA

Loading...
Siku ya Jumatano, jarida la Forbes lilitoa orodha ya wanamuziki wa Hip Hop matajiri duniani ya mwaka 2018, na Jay-Z aliongoza katika orodha hiyo akiwa na jumla ya utajiri wa dola za Kimarekani milioni $900.

Mbinu zake za utafutaji pesa ndio zimemuwezesha kumshusha namba moja mkongwe Sean "Diddy" Combs , ambaye alikuwa akishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka saba mfululizo.

Jay-Z utajiri wake kwa sasa umepanda kutoka dola za kimarekani milioni $810 hadi milioni $900, baada kuongeza mapato yake kwa kuuza zaidi pombe zake aina ya champgne kwa majina Armand de Brignac na D'Usse cognac. Pia ana umiliki mkubwa wa Roc Nation na mtandao wa Tidal.

Diddy kwa sasa ameshushwa mpaka nafasi ya pili, akiwa na jumla ya utajiri wa dola za kimarekani milioni $825, wakati Dr. Dree akiendelea kutetea nafasi yake ya tatu (3) baada ya utajiri wake kuongezeka kutoka dola za kimarekani milioni $740 hadi milioni $770.

Rapper Eminem na Drake wakishikilia nafasi ya nne na tano kwenye tano bora kila mmoja akiwa na jumla ya utajiri wa dola za kimarekani milioni $100.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
ORODHA YA WANAMUZIKI WA HIP HOP MATAJIRI 2018 - JAY Z AONGOZA ORODHA YA WANAMUZIKI WA HIP HOP MATAJIRI 2018 - JAY Z AONGOZA Reviewed by By News Reporter on 3/02/2018 12:51:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.