Loading...

MAHAKAMA YAMTAKA MWIMBAJI AKON KULIPA KIASI CHA MILIONI 340 KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

Loading...
Kwa kushindwa kulipa kodi, mwimbaji Akon mahakama imemuamuru kulipa kiasi cha dola za kimarekani $164,786.99 sawa na pesa za Kitanzania Tshs. 340 Milioni kwa kampuni iliyompangisha sehemu ya ofisi ghorofa ya 66 katika jengo la Empire State kwa ajili ya biashara yake ya maswala ya Mitindo, huko Aliaune Milano.

Kwa mujibu wa nakala ya mashtaka zilizopatikana na mtandao wa TMZ, GTFM kama kampuni iliyompangisha mwimbaji huyo, walidai Akon alikubali kulipa kodi ya kiasi cha dola za kimarekani $25,000 kwa mwezi na alilipa hadi 2015 ndipo alisimama kulipa kodi, GFTM walidai Akon aliondoka rasmi katika jengo hilo mnamo mwaka 2016, akidaiwa jumla ya miezi saba.

Kampuni ya GFTM walimshtaki Akon, lakini mwimbaji huyo hakuwahi kufika mahakamani, hivyo hakimu aliamua kutoa hukumu ya moja kwa moja.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MAHAKAMA YAMTAKA MWIMBAJI AKON KULIPA KIASI CHA MILIONI 340 KWA KUSHINDWA KULIPA KODI MAHAKAMA YAMTAKA MWIMBAJI AKON KULIPA KIASI CHA MILIONI 340 KWA KUSHINDWA KULIPA KODI Reviewed by By News Reporter on 3/02/2018 01:54:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.