Loading...

KENYA: MADAKTARI WASIMAMISHWA KAZI BAADA YA KUMFANYIA UPASUAJI WA KICHWA MGONJWA ASIYESTAHILI

Loading...
Madaktari Hospitali ya Kenyatta wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.

Taarifa kutoka mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, zinabainisha kuwa wagonjwa wawili waliokuwa hawajitambui na mmoja kati yao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu ilionekana imeviria.

Lakini pia mkurugenzi huyo ameomba radhi na kusema "tunafurahi kuwatangazia umma kwamba mgonjwa huyo sasa ametibiwa na anaenedelea vizuri"

Wafanyakazi wanaochunguzwa katika sakata hilo ni pamoja na daktari wa upusuaji wa ubongo, muuguzi, mtalaam wa dawa za usingizi.

Hili sio sakata la kwanza kukumba hospitali hiyo, mwezi wa kwanza mwaka huu, waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliamrisha uchunguzi ufanyike baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.

Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao zilidai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.

Tukio hilo liliibua maandamano na wanaharakati na wanawake walikasirishwa na usalama duni na utendaji kazi wa hospitali hiyo.

Kwa upande wa Tanzania, sakata kama hili liliwahi tokea mwaka 2007.

Tarehe 8 Novemba, madaktari wawili wa upasuaji wa ubongo katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili walimpasua kichwa Emmanuel Didas kutoa uvimbe ambao haukuwepo.

Wakati mgonjwa Emmanuel Mgaya, aliyekuwa na uvimbe huo alipasuliwa goti.

Madaktari hao walichukuliwa hatua na kufutwa kazi na mamlaka ya hospitali.

Lakini jopu la madaktari wamejitokeza kupinga usimamizi huo na kudai kwamba kosa lilianzia kwa wauguzi katika wadi ya kupokea na kuwapanga wagonjwa kwa ajili ya upasuaji na sio daktari aliyefanya upasuaji huo.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za afrika mashariki punde zinapojiri.
KENYA: MADAKTARI WASIMAMISHWA KAZI BAADA YA KUMFANYIA UPASUAJI WA KICHWA MGONJWA ASIYESTAHILI KENYA: MADAKTARI WASIMAMISHWA KAZI BAADA YA KUMFANYIA UPASUAJI WA KICHWA MGONJWA ASIYESTAHILI Reviewed by By News Reporter on 3/02/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.