Loading...

PRODUCER P-FUNK: S2KIZZY, T TOUCH NA LUFFA ACHENI TAARABU

Loading...
Producer mkongwe Bongo, P Funk Khalfani Majani amefunguka kuhusu kuwepo kwa bifu miongoni mwa ma-producer wapya wa sasa.

P Funk ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wao kama ma-producer wanaheshimiana na suala la malumbano mara nyingi ni kwa wasanii na si kwao kwani kwa upande wa production wapo wachache.

“Labda hao wadogo ambao juzi kati nimeona wanalumbana, sijui S2kizzy, T Touch na Luffa, sijui wanasema muziki wa T Touch wa kizamani, kitu kama hicho ni tunacheza taarab sasa,” amesema.

“Kwa sababu kinachoonekana ni kazi, kama muziki umekubali basi ni mzuri uwe wa kizamani au wa kisasa,” amesisitiza.

Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa ni ma-producer ambao kwa sasa kila mmoja anafanya vizuri hapa Bongo, wote kwa sasa ngoma walizofanya vinafanya vizuri katika radio station mbali mbali.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
PRODUCER P-FUNK: S2KIZZY, T TOUCH NA LUFFA ACHENI TAARABU PRODUCER P-FUNK: S2KIZZY, T TOUCH NA LUFFA ACHENI TAARABU Reviewed by By News Reporter on 3/08/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.