Loading...

RAIS MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI VIFO VYA WATU 26 PWANI

Loading...
Rais John Magufuli, ametuma salam za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kutokana na vifo vya watu 26 vilivyotokea juzi katika ajali baada ya basi dogo kugongana na lori lililokuwa limebeba chumvi katika Kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

“Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea,” amesema Rais Magufuli katika taarifa yake.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyoshughulikia usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili huku akiwaombea majeruhi wa ajali hiyo wapone haraka na kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Katika salam zake Rais Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya vifo hivyo na kuongeza kuwa tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvukazi ya Taifa.
Na Geofrey Okechi.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
RAIS MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI VIFO VYA WATU 26 PWANI RAIS MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI VIFO VYA WATU 26 PWANI Reviewed by By News Reporter on 3/26/2018 09:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.