Loading...
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefanya ziara yake ya kwanza nchini Zimbabwe wakati nchi hiyo ikiwa katika malalamiko yanayofanywa na rais wa zamani Robert Mugabe kuwa rais mpya wa Zimbabwe yuko madarakani kinyume na sheria.
Viongozi wote wawili wa Zimbabwe na yule wa Afrika Kusini wameingia madarakani baada ya marais wa nchi hizo kujiuzulu.
Ramaphosa kabla ya kuondoka kuelekea Harare amewaambia waandishi wa habari kuwa hizi ni zama mpya na zama mpya zinahitaji umakini na uvumilivu.
Mnamo mwezi Novemba mwaka jana Robert Mugabe aliachia ngazi kama rais wa Zimbabwe baada ya jeshi kuingilia kati.Mugabe anakiita kitendo hicho mapinduzi.
Mwezi Februari mwaka huu,Zuma aliyaachia madaraka baada ya kutishiwa kushtakiwa na chama chake ANC.
Ardhi ni suala nyeti nchini Afrika Kusini, ambapo rasilimali nyingi bado ziko mikononi mwa wakulima wachache wazungu.
Ramaphosa amesema kuwa suala la ardhi litachukuliwa mfano kutoka Zimambwe ambapo nchi hiyo iliwanyanganya wazungu ardhi kuanzia mwaka 2000,hali iliyopelekea mavuno duni ikifuatiwa na ukame kwa wingi.
Na Fatma Pembe - Dar es salaam.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.

RAIS MPYA WA AFRIKA KUSINI AFANYA ZIARA YAKE YA KWANZA ZIMBABWE
Reviewed by By News Reporter
on
3/18/2018 11:29:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: