Loading...

SERIKALI YA UINGEREZA YARUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA TIBA

Loading...
Wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka 6, Alfie Dingley aliye na ugonjwa wa kifafa ambao wamekuwa wakipiga kampeni ili mtoto wao aruhusiwe kutumia mafuta ya Bangi kupunguza matatizo ya kifafa, wamesema sasa serikali ya Uingereza imekubali kuwapa ruhusa ya kutumia bangi hiyo kama tiba.

Wakiongea baada ya mkutano na Waziri Mkuu Theresa May, Drew Dingley na Hannah Deacon walisema wamefahamishwa kuwa kijana wao Alfie anaweza kuruhusiwa kutumia mafuta yatokanayo na mmea Bangi kwa makubaliano maalumu ingawa matumizi ya Bangi ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Alfie Dingley huanguka kifafa hata mara mia moja na zaidi kila mwezi lakini hali hiyo inaweza kupungua ikiwa atapewa matone matatu ya bangi kwenye ulimi kila siku.

Mama mzazi wa mtoto huyo ameelezea tabu anazozipata, jaziba na hasira ambazo mtoto huyo anamfanyia kutokana na matatizo ya maradhi yake ya kifafa.Ameongeza kuwa watu 380,00 wanaunga ombi hilo na wamewapigia simu familia yao wakidai kuwa wanaridhia wapewe leseni kwaajili ya Alfie Dingley kutumia bangi kwa matibabu.

Hannah Deacon amesema kuwa wamekuwa wakiletewa misokoto mingi ya bangi,watu wakisema wanaelewa tatizo la mtoto.

Hivyo najua wenye mamlaka hawaonji mateso ya maisha ninayo ishi,na wala hawaishi maisha na shida mwanangu,naomba waweke wazi jambo hili.

Muigizaji Sir Patrick Stewart amemwambia mwandishi wa gazeti la Daily Politics Greg Dawson kwamba kwanini anaunga mkono kampeni hiyo.
Na Catherine Kisese


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za afya punde zinapojiri.
SERIKALI YA UINGEREZA YARUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA TIBA SERIKALI YA UINGEREZA YARUHUSU BANGI ITUMIKE KAMA TIBA Reviewed by By News Reporter on 3/22/2018 08:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.