Loading...

TAHADHARI: WIZI WA FIGO KWA WAMAMA WALIOJIFUNGUA KWA OPERESHENI

Loading...
Kama unamjua mwanamke yoyote ambaye amejifungua kwa operesheni; mjuze taarifa hii kwamba kafanye vipimo vya ultra-sound ili kuangalia kama figo yake imebaki salama. Kuna kesi mbili zimetokea za waizi wa figo moja nchini Kenya, Nairobi, ambapo mwanamke mmoja aligundua kwamba anafigo moja baada ya miaka kupita tangu ajifungue mtoto wake.

Mama huyo alidai kwamba wakati operesheni yake ya kujifungua ndipo madaktari kutoka katika hospitali moja hapo Nairobi ndipo walipotumia fursa ya kuiba figo yake moja na kumuuzia mgonjwa mmoja hospitalini hapo.

Kesi nyingine ilitokea hivi karibuni huko Zambia baada ya mwanamke mmoja mwanamuziki alipogundua ana figo moja, baada ya miezi kadhaa kupita tangu kujifungua kwake. Chanzo karibu kilielezea kuwa mwanamke huyo alianza kusikia maumivu makali tangia siku amefanyiwa operesheni hiyo kwa mfumo wa C-Section, ndipo aliposhauriwa kufanya SCAN ili kufahamu kama anafigo zote lakini ikutwa moja moja ilikwishatoweka.

Hivi vitendo kwa sasa imekuwa kawaida na hii ni kutokana bei ya figo zinavyouzwa hata kuwaperekea madaktari waliokosa uadilifu kuingiwa tamaa na kutekeleza wizi huo.

Kwa sasa bei ya figo moja inafika mpaka Mil 400 kwa pesa za kitanzania. Hii inamaanisha madaktari wanatengeneza pesa nzuri kupitia wizi huo.
Na Fatma Pembe
TAHADHARI: WIZI WA FIGO KWA WAMAMA WALIOJIFUNGUA KWA OPERESHENI TAHADHARI: WIZI WA FIGO KWA WAMAMA WALIOJIFUNGUA KWA OPERESHENI Reviewed by By News Reporter on 3/22/2018 09:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.