Loading...
Sasa hivi kumekuwa na matapeli ambao wanakupigia simu na kuomba kufanya kazi na wewe.
Hawa jamaa ni wasomi, wataalamu na pia wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kukushawishi ili ukubali kufanya nao kazi na pia kuwapa pesa.
Imegundulika kuwa mtandao wa matapeli ndani yake wapo wasomi wakubwa wa vyuo vikuu, madaktari, walimu na watu wenye nyadhifa mbalimbali katika ofisini binafsi na hata za serikali.
Pia ukumbuke kwamba kama watakuwa wameamua kukupiga pesa ndefu na kutokana na aina ya kazi waliokusomesha kufanya nao basi wajanja hawa huwatumia matapeli wenzao walioko nchi za nje kukupigia simu na namba za USA, Canada, India au nchi yeyote ili kukutengenezea mazingira mazuri ya wewe kutoa pesa.
Mara nyingi matapeli hawa hushughulika na kazi zifuatazo.
1. Kutafutia watu kazi jeshini na kampuni mbalimbali zinazitambulika kabisa kimataifa au kiserikali.
2. Kujifanyana wao ni kampuni kubwa Marekani inataka kufungia branch yake Tanzania na hapa utapigiwa simu na mzungu wao alioko Marekani.
3. Wanaweza kukupa dili ya kupokea watalii na kukupa dili ya kutengeneza vivutio vya watalii kama Masai Shuka, bangili.
4. Wanaweza kukupa dili ya kupokea tenda za
serikali kuhusu kilimo na hapa utapigiwa simu na anaependa kujitambulisha yeye ni Afisa Kilimo wa Rufiji
5. Watu hawa hununua vitu mbali mbali katika maduka na hapa watakueleza kuwa twende bank tukakulipe na wakati huo mshapakiza mzigo katika gari inawasubiri nje ya bank lakini wanatabia ya kupaki bank sehemu isioruhusiwa, yani wrong parking, na wanapenda sana bank za CRDB au NMB kwenye foleni kubwa, sasa akiwa kwenye foleni kubwa utaona askari anaingia na bunduki na kitangaza gari aina fulani imepaki ktk mlango wa bank tafadhali mwenye gari kasogeze, basi tapeli huyu atakuomba wewe ukae katika foleni ili yeye akasogeze gari na hapo utakaa hadi bank ifungwe yeye hutamuona tena.
6. Kwa wale kwenye kutafuta viza matapeli hawa wako huko.
7. Ukiwa umelazwa katika Hospital za rufaa na ukapewa barua ya kupelekwa nje, utashangaa utapigiwa simu na namba kutoka India na hapo wataanza kuongea Kihindi msipoelewana utaona badae anapiga mtu wa hapa anakueleza kuwa ulipigiwa simu yeyote kutoka India? Ukijibu ndio anasema yeye ni wakala wa Hospital unaotakiwa kwenda kutibiwa hivyo unaweza kufanya malipo hapa hapa, ukizubaa tu unatapeliwa na hawana hata huruma we ni mgonjwa.
8. Matapeli hawa wana mtandao wao katika internet wa vikoba ambapo wanakopesha hela kwa kutumia jina la mheshimiwa Zitto Kabwe au mama salma kikwete ukishajaza form yao utapigiwa simu ili kufanya malipo ya awali na pia watakuunganisha katika group lao LA WhatsApp ambao huko utakutana na watu wengi sana wakishukuru msaada wanaopewa na Zitto Kabwe au mama salma kikwete ili kukushawishi wewe kutuma pesa za awali, ukituma tu umepigwa.
Tuwe makini sana Watanzania tusiibiwe hovyo na sambaza ujumbe huu kwani kila dakika kuna mtu anatapeliwa sehemu fulani msaidie haraka sana asitapeliwe.
Hizi ni baadhi ya namba wanazotumia kwa hapa Tanzania
0768 020 273
0788 177 313
0758 268 896
Kumbuka kwamba wakishaamua kukutapeli wana taarifa zako zote na wanakujua vizuri sana hilo lisikupe shida ukaingia mkenge…
USHAURI:
1.Fanya kazi au kubali wito na mtu unayemjua na kumwamini.
2. Usitoe pesa yoyote haraka bila kujiridhisha na hiyo kazi au hiyo Biashara.
3. Andikishana mikataba ya kisheria kabla ya Biashara yoyote kuanza.
4. Usimuachie mali yako mtu yeyote yule kama humuamini au hata kama unamuamini.
5. Usipende kuchukulia maisha au mambo kirahisi rahisi itakucost.
6. Pata elimu sahihi ya lifeskills na self defence ktk maisha.
7.Akili za kuambiwa changanya na zako.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata tahadhari punde zinapojiri.
TAHADHARI: UMEINGIA MTINDO MPYA WA UTAPELI
Reviewed by By News Reporter
on
3/11/2018 01:32:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: