Loading...

PAPII KOCHA AMEMSAMEHE MKE WAKE KWA KUOLEWA NA MTU MWINGINE

Loading...
Papi Kocha amasema amemsamehe mke wake kwa kuolewa na mwanaume mwingi wakati alipokuwa jela akitumikia kifungo cha maisha.

Kocha, ambaye alifungwa pamoja na baba yake Nguza Viking, aliachiliwa huru kwa msamaha wa rais siku ya Sikukuu za Uhuru Disemba 9, 2017.

Wawili hao walifungwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na kosa kuwalawiti watoto 10 wa shule ya msingi.

Lakini, Papii Kocha akiiambia televisheni moja hapa nchini siku ya Ijumaa, Machi 9, kwamba mke wake ameolewa na mwanaume mwingine na hamtupii lawama.

"Nimekaa miaka 14 jela sio utani! Tulibahatika kupata watoto ambao wanatuunganisha. Mtoto wangu alikuwa na miaka minne wakati nafungwa jela na wakati natoka sasa anamiaka 18," alisema Kocha.

Bw Nguza na watoto wake wa kiume watatu walifungwa jela Octoba 12, 2003 wakiwa katika nyumba yao iliyoko sinza karibu na shule ambapo wanafunzi hao walikuwepo.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
PAPII KOCHA AMEMSAMEHE MKE WAKE KWA KUOLEWA NA MTU MWINGINE PAPII KOCHA AMEMSAMEHE MKE WAKE KWA KUOLEWA NA MTU MWINGINE Reviewed by By News Reporter on 3/11/2018 01:53:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.