Loading...

UGONJWA WA 'DENGUE' UMEREJEA NCHINI BAADA YA WAGONJWA 11 KUGUNDULIKA

Loading...
Ugonjwa wa Dengue umerejea nchini baada ya wagonjwa 11 kugundulika katika Hospitali ya Ocean Road

Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imeeleza kuwa homa ya ugonjwa huo imegundulika baada ya wagonjwa kadhaa waliokuwa na dalili zake kupimwa na kuthibitishwa

Mara ya kwanza ugonjwa huo uligundulika mwaka 2014 ambapo wagonjwa 400 waliupata. Walitibiwa na kupona, isipokuwa watatu ndiyo walifariki dunia

Tahadhari imetolewa kwa wananchi kupima afya haraka wanapohisi wana homa Kali, mafua na kuumwa kichwa kwa muda, ambazo ni dalili kubwa za homa ya dengue

Vimelea vya ugonjwa wa homa ya dengue husambazwa na mbu kama ilivyo kwa malaria. Hivyo wananchi wanahimizwa kuua mazalia ya wadudu hao haraka.

Na Geofrey Okechi - Dar es salaam.

Tuma neno 'AFYA' kwenda +255765112259 kupata habari za AFYA punde zinapojiri.
UGONJWA WA 'DENGUE' UMEREJEA NCHINI BAADA YA WAGONJWA 11 KUGUNDULIKA UGONJWA WA 'DENGUE' UMEREJEA NCHINI BAADA YA WAGONJWA 11 KUGUNDULIKA Reviewed by By News Reporter on 3/20/2018 08:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.