Loading...

UJUMBE MZITO ALIONDIKA 'TUNDU LISSU' KUHUSU VIONGOZI WA CHADEMA

Loading...
"Ni ajabu iliyoje kwamba katika Wiki ya Pasaka, wiki ambayo Yesu Kristo alitiwa kifungoni na baadae kuuawa msalabani, Serikali ya Magufuli imeamua kwamba viongozi wote wa juu CHADEMA wakamatwe kama alivyokamatwa Yesu Kristo; washtakiwe kama alivyoshtakiwa Yesu Kristo; na wasulubiwe kwa kuwekwa mahabusu kama alivyosulubiwa Yesu Kristo msalabani.

"Pontio Pilato aliyehukumu kesi ya Yesu Kristo alisema haoni kosa lake. Hata hivyo, bado Yesu Kristo akasulubiwa na askari wa Kirumi na kufia msalabani.

"Hakimu Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi ya Mwenyekiti Mbowe na wenzake, amesema wanastahili kupata, na amewapa, dhamana.
Askari polisi wa Magufuli, kama ilivyokuwa kwa askari wa Kirumi wa Kaisari, wameamua kutokuwaachia na kuwalazimisha kuwa kifungoni wakati huu wa Pasaka.

"Wanafanya hivyo kwa kufikiria kwamba wanawakomesha. Hawajui watendalo na Mungu awasamehe pamoja na waliowatuma.

"Kuendelea kuwafunga watu ambao Mahakama imesema wapewe dhamana sio kuwaadhibu, bali ni kuwapa upako mkubwa wa kisiasa mbele ya wananchi. Ni kuwafanya wahanga wa ukombozi wa pili wa nchi yetu.

"Magufuli ameomba kuombewa kwa Mungu mara nyingi. Kwa matendo haya ya Jeshi la Polisi, ni kweli anastahili kuombewa", aliandika kupitia mtandao wa kijamii.
Na Peter Godwin.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za siasa punde zinapojiri.
UJUMBE MZITO ALIONDIKA 'TUNDU LISSU' KUHUSU VIONGOZI WA CHADEMA UJUMBE MZITO ALIONDIKA 'TUNDU LISSU' KUHUSU VIONGOZI WA CHADEMA Reviewed by By News Reporter on 3/31/2018 05:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.