Loading...

WAITALIA WANAPIGA KURA KUICHAGUA SERIKALI MPYA

Loading...
Waitalia leo wanapiga kura kuichagua serikali mpya katika uchaguzi ambao unahofiwa huenda ukasababisha mkwamo wa kisiasa baada ya kipindi cha kampeinii kilichoshuhudia ghadhabu ya wapiga kura kuhusu uchumi mbaya, kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira na suala la uhamiaji.

Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unabashiri kuwa chama cha waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi na washirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia huenda wakanyakua viti vingi vya bunge lakini watashindwa kupata viti vya kutosha kuunda serikali. 

Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja asubuhi hadi saa tano usiku, na matokeo ya awali yatatangazwa punde baada ya vituo kufungwa. Matokeo kamili yanatarajiwa hapo kesho.

Berlusconi mwenye umri wa miaka 81 aliyelazimika kujiuzulu kama waziri mkuu mwaka 2011 amerejea katika ulingo wa kisiasa nchini Italia kwa kishindo. 

Hata hivyo kutokana na kukutikana na makosa mwaka 2013, ya ukwepaji kodi, haruhusiwi kushikilia wadhifa wa uongozi, hivyo anampigia debe Antonio Tajani, Rais wa bunge la Ulaya kuwa waziri mkuu.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
WAITALIA WANAPIGA KURA KUICHAGUA SERIKALI MPYA WAITALIA WANAPIGA KURA KUICHAGUA SERIKALI MPYA Reviewed by By News Reporter on 3/04/2018 09:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.