Loading...

WASANII WATAKAOSHIRIKIANA NA DIAMOND PLATINUMZ KUTUMBUIZA FIFA 2018 NCHINI URUSI

Loading...
Mwimbaji Ykee Benda ametajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki kutoka barani Afrika kwamba atatumbuiza katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 linalotarajia kufanyika nchini Urusi. Mwimbaji huyo alithibitishwa jana wakati wa ziara ya FIFA kombe la dunia iliyofanyika nchini Uganda chini ya udhamini wa kampuni ya Coca Cola.
 Lizha James - Kutoka Msumbiji.
Sami Dan - Kutoka Ethiopia.
Tanzania, Uganda, Ethiopia, Msumbiji na Afrika Kusini ndio nchi pekee zilizochaguliwa kupereka wanamuziki watakaotumbuiza katika ufunguzi wa michuano hiyo.

Hapa nchi atatuwakilisha msanii Diamond Platinumz, Uganda ni YKee Benda, Ethiopia watawakilishwa na msanii Sami Dan na James atawakilisha Msumbiji.

YKee Benda ametokea kuvuma sana kuanzia mwaka 2017 na kuonekana kufanya vizuri zaidi mwaka huu, mwimbaji huyu atakuwa wa pili nchini Uganda kutumbuiza katika michuano ya FIFA Kombe la Dunia baada ya msanii Jose Chameleone ambaye alitumbuiza mwaka Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
WASANII WATAKAOSHIRIKIANA NA DIAMOND PLATINUMZ KUTUMBUIZA FIFA 2018 NCHINI URUSI WASANII WATAKAOSHIRIKIANA NA DIAMOND PLATINUMZ KUTUMBUIZA FIFA 2018 NCHINI URUSI Reviewed by By News Reporter on 3/07/2018 10:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.