Loading...

WATU 16 WAMEFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI - RWANDA

Loading...
Angalau watu 16 wamekufa na mamia kujeruhiwa kwa radi iliyopiga kanisa moja la Wasabato huko Rwanda, Taarifa zimeelezwa na tawala za mitaa, jana Jumapili.

Watu 14 walifariki papo hapo baada ya radi kupiga katika kanisa hilo lililopo katika Wilaya ya Nyaruguru Kanda ya Kusini siku ya Jumamosi, Meya wa mtaa Habitegeko Francois aliitaarifu AFP kupitia simu.

Wawili wengine walifariki baadae kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata, alisema.
Aliongezea kwamba watu 140 waliohusika katika tukio hilo walifikishwa katika hospitali ya Wilaya, lakini wengi wao wamesharuhusiwa.

"Daktari amesema watatu tu kati yao ndio wana hali mbaya lakini wengine wanaendelea vizuri," alisema.

Kwa mujibu wa meya, tukio kama hilo lilitokea siku ya Ijumaa, ambapo radi iliwapiga wanafunzi 18 na kwa bahati mbaya ilimuua mmoja wao.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
WATU 16 WAMEFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI - RWANDA WATU 16 WAMEFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI - RWANDA Reviewed by By News Reporter on 3/12/2018 08:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.