Loading...

BINTI WA RAIS MUSEVENI ADAI MUNGU ALIMTOKEA AKIWA NA MIAKA 11 NDIPO AKAAMUA KUOKOKA

Loading...
Binti wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Patience Rwabwogo amefunguka na kusema kwanini aliokoka akiwa umri mdogo na sababu iliyomfanya awe mhubiri.

Akiwahutubia waumini katika kanisa la Worship House Nansana, Rwabwogo alisema kuwa Mungu alimtokea katika ndoto na kumwambia kwamba atakuwa nuru katika nchi ya Uganda na Afrika nzima.

"Kila siku nilikuwa nikionyeshwa jinsi Afrika ilivyojaa kiza, nilikuwa nikisikia sauti ikisema,'Kwenye giza kutakuja kuwa na nuru ya ajabu', Kisha nikamuona mtu akipiga tarumbeta na nuru ikatokeza Uganda," Rwabwogo alisema.

"Mungu alisema, kila mara huwa unajiangalia kimwili lakini nuru ipo ndani yako na nuru hiyo inaangaza kabisa na itasambaa kwa mataifa mengine," Rwabwogo aliongezea.

Rwabwogo alisema alimuuliza Mungu mbona mwangaza ulikuwa ukitoka Uganda na akamjibu kuwa, ni nchi ambayo iliteuliwa kwa roho ya Afrika nzima.

Rwabwogo aliamua kuokoa akiwa na umri wa miaka 11 na kufungua kanisa lake la The Covenant Nation Church mwaka 2006 ambapo amekuwa akiubiri hadi leo.
Na Catherine Kisese.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
BINTI WA RAIS MUSEVENI ADAI MUNGU ALIMTOKEA AKIWA NA MIAKA 11 NDIPO AKAAMUA KUOKOKA BINTI WA RAIS MUSEVENI ADAI MUNGU ALIMTOKEA AKIWA NA MIAKA 11 NDIPO AKAAMUA KUOKOKA Reviewed by By News Reporter on 4/12/2018 10:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.