Loading...

MWILI WA MWANAMKE ULIOZIKWA WATOWEKA KWENYE KABURI

Loading...
Wanakijiji wa Bolo maeneo ya Nyakach katika kata ya Kisumu walishikwa na bumbuwazi siku ya Jumatatu asubuhi baada ya kukutwa mwili wa mwanamke mmoja waliouzika miaka miwili iliyopita kutoweka katika kaburi.

Msichana Joyce Auma alizikwa miaka miwili iliyopita.

Lakini kwa mujibu wa Bwana Benjamin Rambogo, mjomba wa bi Auma,wanakijiji walikuta jeneza tupu katika kaburi lililokuwa wazi.

Jumatano, wanakijiji hao walioshtusha waliendelea kujiuliza kwanini kaburi, ambalo lipo umbali kidogo na nyumba za familia ya marehemu, lilifukuliwa.

Bw. Michael Okello, baba wa marehemu, alisema hakukuwa na migogoro yoyote kuhusu ardhi wala mahali pa kuzikia, labda wahalifu wametenda tukio hilo.

"Bi. Auma aliishi na mabwana watatu bila kufunga nao ndoa, bwana wake wa kwanza ambaye alimtelekeza hakuhudhuria katika mazishi yake wala kuulizia mwili wake," alisema Bwana Okello.

Bi Auma alikuwa na ndoa za utata, baba yake alisimulia.

Shemeji zake waliokuwa wanaishi kata ya Migori walimnyang'anya mali zake na kumfukuza baada ya kifo cha mumewe wa kwanza 2011.
Na Mohammed Makame.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za matukio punde zinapojiri.
MWILI WA MWANAMKE ULIOZIKWA WATOWEKA KWENYE KABURI MWILI WA MWANAMKE ULIOZIKWA WATOWEKA KWENYE KABURI Reviewed by By News Reporter on 4/12/2018 10:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.