Loading...

CHAMELEONE MATATANI KUSHIKWA NA POLISI KWA KUWARUHU WATOTO WAKE WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 KUENDESHA GARI BARABARANI

Loading...
MWANAMUZIKI tajiri na mkongwe nchini Uganda, Jose Chameleone yupo mashakani baada ya polisi wa usalama barabarani (Traffic) nchini humo kumtaka afafanue ni kwa nini aliwaruhusu watoto wake wa kiume kuendesha gari bila ya uangalizi wake.

Video ya watoto hao ilisambaa katika mitandao ya kijamii ndipo polisi wakachukua hatua madhubuti kuhusu tukio hilo, imeripotiwa kuwa kwa mara ya kwanza video hiyo ilirushwa mtandaoni na Chameleone mwenyewe, kama njia ya kuonyesha ufahari juu yake.
"Damn!! Abba Marcus na Alfa Mayanja kanyageni. Watoto wangu wanakua haraka sana," Chameleone aliandika chini ya video hiyo na kuitupia mtandaoni Jumatano, Aprili 11.

Kuna waliomsifu kwa video hiyo na walidai ni bora anayewajali na kuwapa watoto wake maisha bora, ingawa kuna ambao hawakupendezwa na kitendo hicho kwani aliwapa gari vijana ambao hawana uelewa mwingi na maswala ya barabarani na vyombo vya moto na hata kusema ni kinyume na sheria.

Kwa sasa nyota wa kibao cha 'Valu valu' ana kibarua kigumu kuwaelewesha polisi ni kwanini alifanya hivyo.

Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda Polisi wa Trafiki Kampala, Norman Musinga alisema mwanamuziki huyo amevunja sheria na huenda akakamatwa na akatozwa faini.

Watoto wa msanii huyo ni wa umri wa miaka 14 na 9 wanafunzi na walikuwa wakiliendesha gari la baba yao aina ya 'Bentley Open Convertible' katika barabara kuu ya Entebbe Express.
Na Godwin Mbaningo



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
CHAMELEONE MATATANI KUSHIKWA NA POLISI KWA KUWARUHU WATOTO WAKE WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 KUENDESHA GARI BARABARANI CHAMELEONE MATATANI KUSHIKWA NA POLISI KWA KUWARUHU WATOTO WAKE WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 KUENDESHA GARI BARABARANI Reviewed by By News Reporter on 4/15/2018 04:14:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.