Loading...

HUYU NDIYE 'NABII' ANAYEDAIWA KUBADILI MAJI KUWA PETROLI

Loading...
Mojawapo ya miujiza aliyofanya Yesu Kristu ni kubadilisha maji kuwa divai katika harusi iliyofanyika Canan na hii ni kwa mujibu wa Kitatu Cha Yohana katika Bibilia.

'Muujiza' kama huo unadaiwa kufanyika Aprili 3 huko nchini Kenya, kata ya Bungoma, wakati mtumishi mmoja wa Mungu anayeaminiwa kutokea Afrika Kusini, alipoyageuza maji na kuwa mafuta ya petroli na sio divai wakati wa maadhimisho ya Pasaka.

Inataarifiwa kuwa, Nabii Jacob aliwaomba wafuasi wake kuja na chupa zenye maji na aliyageuza maji hayo na kuwa petroli

Kulingana na ujumbe wake binafsi aliourusha kupitia ukurasa wake wa facebook, nabii huyo wakujiita, alianza kwa kuwauliza wafuasi wake kama wanaamini anaweza kubadili maji kuwa petroli.
"Mnaamini tunaweza kubadili maji kuwa petroli?" aliuliza.

Ndipo Jacob akaombea maji hayo na wakati akiombea maji, inadaiwa ghafla maji yalibadilika na kuwa petroli na kuanza kushika moto.

Hata hivyo, wengi hawaani kuwa maji yalibadilika na kuwa mafuta ya petroli na kwamba muujiza huo ni batili au wa mazingaombwe ili watu waweze kujiunga.
Na Fatma Pembe.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za matukio punde zinapojiri.
HUYU NDIYE 'NABII' ANAYEDAIWA KUBADILI MAJI KUWA PETROLI HUYU NDIYE 'NABII' ANAYEDAIWA KUBADILI MAJI KUWA PETROLI Reviewed by By News Reporter on 4/11/2018 08:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.