Mwanamuziki nyota nchini Marekani, Jay-Z amesema alilia kwa faraja mara baada ya kuthibitishwa na mama yake kuwa yeye ni shoga.
"Nilijawa na furaha kwa ajili yake kwamba amekuwa huru," mwanamuziki huyo alimweleza David Letterman katika kipindi chake kipya cha Netflix.
Jay-Z, katika kipindi hicho aliimba kwa mtindo wa kufoka foka wimbo wake wa Smile, uliopo kwenye albamu 4:44.
"Mama ana watoto wanne, lakini ni msagaji/ aliishi maisha ya kuigiza. Alikuwa akijificha ndani ya kabati, kwa hiyo alikuwa akiishi maisha ya aibu mbele ya jamii huku maumivu yakiwa makubwa sana kuyabeba."
Lakini sasa mwanamuziki huyo mwenye miaka 47 amesema ana furaha kubwa baada ya kuujua ukweli kuhusu mama yake kuishi maisha ya kupendwa tena.
"Hebu fikiri unaishi maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine. Na kudhani kwamba unawalinda wanao," Jay-Z alisema hayo katika utambulisho wa shoo yake ya My Next Guest Needs No Introduction.
"Mama yangu alipokaa mbele yangu na kuniambia, nadhani ninampenda mtu fulani. Kwa kweli nililia sana."
Amesema, mazungumzo hayo yamefanyika kati yake na mama yake miezi minane iliyopita, wakati akirekodi albamu yake.
"Nilikuwa nikilifahamu hilo. Lakini ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kuzungumzia hili ana kwa ana," alisema Jay Z.
Na Neema Joshua.
Hakuna maoni: