Loading...

AFRIKA KUSINI: RAMAPHOSA AMLILIA 'WINNIE MANDELA', ASEMA ALIKUWA MFANO WA KUIGWA

Loading...

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametuma salaam za rambirambi kufuatia kifo cha mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Mandela kilichotokea mapema jana Jumatatu.

Ramaphosa akihutubia vyombo vya habari baada ya kutembelea nyumbani kwa Mandela katika kitongoji cha Soweto jijini Johannesburg, amesema wananchi wote wa Afrika Kusini wanaomboleza kifo cha Winnie Mandela.

"Tulikua tukiangalia namna Winnie alivyojiendesha mwenyewe kwa kukabiliana na aina mbaya na ya kutisha ya ubaguzi wa rangi. Winnie Mandela siyo kwamba alikuwa mtu wa mfano wa kuigwa lakini aligusa maisha ya mamilioni ya wananchi wa Afrika Kusini wakati wa zama za giza za ubaguzi wa rangi wakati huo Chama cha ANC kilipopigwa marufuku na wananchi kuishi katika shimo la ubaguzi wa rangi.

“Alibaki kuwa sauti pekee ya harakati za kupigania demokrasia. Aliendelea kuonyesha ujasiri dhidi ya aina za kutisha ambazo zilielekezwa kwake na harakati zake.Vuguvugu lake linamkumbuka sana kwa kuwa mmoja wa viongozi ambao vuguvugu letu la ukombozi liliwahi kuwa nao. Alikuwa na uwezo huu mkubwa wa kuwaunganisha wananchi wengi wa Afrika Kusini bila kujali rangi zao au itikadi zao za kisiasa. " 

Naye Kiongozi wa Chama cha Upinzani, Julius Malema ametembelea nyumbani kwa mwanaharakati huyo wa upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi, Winnie Madikizela-Mandela na kusema kifo chake kimeumiza sana.

Wafuasi wa Chama cha Malema cha EFF waliimba na kucheza nje ya nyumba ya familia ya Mandela katika kitongoji cha Soweto.

Ilikuwa ni uchungu sana, ilikuwa kama ndoto kwa sababu Mama alikuwa analazwa na kutoka hospitalini, kwa hiyo niliposikia amelazwa nilijua kuwa atarudi nyumbani, safari hii haikuwa hivyo na nilitambua kuwa ni kweli hayo yametokea wakati familia yake iliponipigia simu. Kwa hiyo taarifa hiyo ilitisha na tunatakiwa tukubali kwamba alikuwa na umri mkubwa na alikuwa mgonjwa na ameacha jukumu hili mikononi mwetu. Tutaendelea na mapambano kwa sababu hatutaki kumwangusha. "

Winnie Madikizela-Mandela, ambaye alikuwa mke wa pili wa Nelson Mandela kati ya watatu waliowahi kuolewa na kiongozi huyo wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini, atazikwa kwa heshima zote za kitaifa Aprili 14 na kutanguliwa na ibada ya kitaifa Aprili 11 mwaka huu.

Na Hamis Fakhi.

AFRIKA KUSINI: RAMAPHOSA AMLILIA 'WINNIE MANDELA', ASEMA ALIKUWA MFANO WA KUIGWA AFRIKA KUSINI: RAMAPHOSA AMLILIA 'WINNIE MANDELA', ASEMA ALIKUWA MFANO WA KUIGWA Reviewed by By News Reporter on 4/04/2018 03:19:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.