Loading...
Bondia Manny Pacquiao ambaye amewahi kuchukua ubingwa wa dunia mara nane katika uzito tofauti, anatarajia kukutana na bondia Lucas Matthyss wa Argentina kuwania mkanda wa WBA Welterweight katika pambano ambalo litapigwa Julai 14, mwaka huu.
Bondia huyo ambaye ni Seneta nchini Ufilipino mwenye umri wa miaka 39, hajapigana tangu alivyoshindwa pambano lake la mwisho alilocheza na Muastralia Jeff Horn na kupoteza mkanda wa WBO mwezi Julai mwaka jana.
Na Catherine Kisese.
MANNY PACQUIAO KUZICHAPA NA BONDIA MUARGENTINA
Reviewed by By News Reporter
on
4/04/2018 03:28:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: