Loading...
Kuna njia mbali mbali za kupika maharage lakini kuna moja haitambuliki sana na watu wengi ingawa inahitajika mpishi awe na subira pale anapotumia mbinu hiyo.
Unachohitaji kuwa nacho ni 'Chupa ya chai au Thermos Flask' pekee na utapika maharage mpaka yaive kwa njia nyepesi na bora zaidi.
Mbinu hii wengi wetu hatuitumii na sio maarufu kwa mapishi ya maharage kama njia nyingine zilizozoeleka ijapokuwa ni bora zaidi na inapunguza gharama za mkaa, gesi, umeme na mafuta ya taa kama nishati za kupikia.
Hatua zifuatazo ni muhimu kwa mapishi ya maharage:-
1. Kwanza, tafuta chupa ya chai (Thermos Flask) ambayo itakuwa na ukubwa sawa na maharage unayotaka kupika.
2. Pima kiwango cha maharage unachohitaji kwa kutumia kikombe.
3. Chemsha maharage hayo kwa muda mfupi kwenye sufuria.
4. Yaweke maharage hayo kwenye chupa hiyo ya chai kisha ufunge kwa nguvu kuzuia hewa kuingia.
5. Yaache kwa muda wa masaa sita kama ni usiku yaache yalale ndani ya chupa hiyo.
6. Baada ya hapo, maharage yako yatakuwa yanafaa kupikwa vizuri kwa viungo kwa ajili ya kula na wali, ugali, maandazi au kama futari.

Na Neema Joshua.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afya punde zinapojiri.
JINSI YA KUPIKA MAHARAGE KWA KUTUMIA CHUPA YA CHAI
Reviewed by By News Reporter
on
4/04/2018 09:01:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: