Loading...

JOHARI ASEMA ATAENDA KWA MAKONDA KUSEMA AMEACHWA

Loading...
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ametoa kali ya mwaka baada kusema kuwa na yeye atakwenda kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kudai kuwa ameachwa wala sio kutelekezewa mtoto au kunyimwa matunzo ya mtoto.

Akizungumza na Risasi Jumamosi Johari alisema, yeye hana shida ya kuachiwa mtoto bali ataenda kusema kuwa aliachwa na mtu ambaye alikuwa akimpenda hivyo aangalie utaratibu ambao na yeye atasaidiwa kama mwanamke aliyeachwa.

“Mimi nitaenda pale lakini tatizo langu ni tofauti kabisa maana mimi ni kuhusiana na kuachwa tu na si vinginevyo” alisema Johari ambaye hakumtaja mtu anayemlenga licha ya kwamba aliwahi kuwa kwenye uhusiano na staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Na Neema Joshua.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
JOHARI ASEMA ATAENDA KWA MAKONDA KUSEMA AMEACHWA JOHARI ASEMA ATAENDA KWA MAKONDA KUSEMA AMEACHWA Reviewed by By News Reporter on 4/15/2018 07:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.