Loading...

PICHA ZA MATUKIO KATIKA MAZISHI YA MAMA WINNIE MANDELA HUKO SOWETO

Loading...
Mazishi ya aliyekuwa mpiganaji dhidi ya ubaguzi nchini Afrika Kusini, Winnie Mandela yamefanyika jana nyumbani kwake Soweto ambako aliagwa na zaidi ya watu 40,000 waliofuraika katika uwanja wa mpira kushuhudia tukio hilo.

Mazishi hayo yalikuwa ni ya kiwango cha juu zaidi kufanywa kwa mtu ambaye si mkuu wa nchi. Marehemu Winnie ambaye alikuwa mke wa aliyekua rais wa kwanza wa Afrika Kusini baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi, Nelson Mandela, alifariki Aprili 2 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 81. Rais Cyrille Ramaphosa wa Afrika Kusini aliongoza mazishi hayo pamoja na familia ya marehemu Winnie.


Salaam za rambirambi zimemiminika kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ambaye alimtaja kama “alama ya kimataifa ya kupinga uonevu”. Winnie Mandela alikulia katika jimbo la Eastern Cape kabla ya kwenda kufanya kazi jijini Johannesburg ambako alikuwa na Nelson Mandela na kuoana mwaka 1958.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
PICHA ZA MATUKIO KATIKA MAZISHI YA MAMA WINNIE MANDELA HUKO SOWETO PICHA ZA MATUKIO KATIKA MAZISHI YA MAMA WINNIE MANDELA HUKO SOWETO Reviewed by By News Reporter on 4/15/2018 07:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.