Loading...

KENYA: MBUNGE ALIYEPENDEKEZA WANAUME WAOE WAKE WENGI AZUA TAHARUKI

Loading...
Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kiambu Gathoni Wamuchoma aliwapendekezea wanaume waoe wake wengi.

Wamuchomba alisema kuwa vijana waliopewa malezi bila baba huishia kunywa pombe na kulewa chakari.

Wakenya waligawanyika kwa maoni yao kuhusu pendekezo la mbunge huyo Wakenya wametoa maoni tofauti kuhusu pendekezo la mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kiambu Gathoni Wamuchomba ambalo liliwashawishi wanaume kuoa wake wengi.

Kituo kimoja cha habari nchini humo kilifanya upekuzi wa maoni ya Wakenya siku ya Jumanne, Aprili 3 na kugundua kuwa Wakenya takriban kwa kiwango sawa waliunga na kupinga pendekezo hilo.

Baadhi ya Wakenya walipendekeza wazo hilo lizingatiwe, sio tu kwa wanaume kutoka eneo la Kati kama mwakilishi huyo wa wanawake alivyopendekeza, bali kwa wanaume wote wa Kenya kukidhi mahitaji ya zaidi ya mke mmoja.
Na Neema Joshua.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
KENYA: MBUNGE ALIYEPENDEKEZA WANAUME WAOE WAKE WENGI AZUA TAHARUKI KENYA: MBUNGE ALIYEPENDEKEZA WANAUME WAOE WAKE WENGI AZUA TAHARUKI Reviewed by By News Reporter on 4/03/2018 12:52:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.