Loading...

KITUO CHA KUZALISHIA VIFARANGA VYA SAMAKI KUZINDULIWA APRILI 20

Loading...
MAKAMU wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha kutotolea vifaranga vya samaki (marine hatchery) huko Beit –el – Raras, hafla itakayofanyika Aprili 20 mwaka huu.

Ofisa wa Mazao baharini Mohammed Soud Mohammed aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko ofIsini kwake Maruhubi.

Alisema kukamilika kwa kituo hicho kutawawezesha kutotoleWa vifaranga vya samaki, kaa na majongoo ya bahari ambao utawapa fursa wafugaji kupata mbegu za kutosha za kuendeleza ufugaji wao.

Hivyo ni vyema kuboresha miundombinu ya ufugaji ikiwemo mabwawa ya samaki, kaa, na majongoo bahari ili kuupokea vifaranga vitakavyotolewa kupata kuongeza uzalishaji wa samaki na mazao mengine ya baharini kwa faida za kijamii, kimazingira na kiuchumi.

Alisema pia, kutaweza kutoa fursa za ajira kwa vijana na kujiongezea kipato ili kuweza kujikimu kimaisha katika kupunguza umaskini nchini.

Aidha alifahamisha kuwa uzalishwaji wa vifaranga hivyo, utaongeza uzalishaji wa kutumia teknologia ya kutotolea vifaranga suala ambalo litaweza kuwatosheleza wafugaji.

Alisema wataongeza pato kwa wananchi pia kutainua pato la taifa katika kuongeza uchumi wa nchi kwa mtu mmoja mmoja na kwa vikundi.

Alisema kuwa vijana wengi wanaojishughulisha na ufugaji wa samaki kaa na majongoo ya bahari watapata fursa za kupata ajira hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo kwa kutayarisha mabwawa yao ya kufugia.

Mohammed alisema serikali ya Mapindizi ya Zanzibar inafanya kila juhudi katika kutatua kero za wananchi, hivyo katika kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa vifaranga vya samaki vinapatikana.

Alisema mradi huo umefadhiliwa na shirika la KOICA na kutekelezwa na shirika la FAO ambapo mradi wa miaka mitatu na umegharimu dola milioni 3,228,103.

Kati ya fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa hatchery, kwa ajili ya vifaa na nyengine kwa ajili ya uendeshaji na kujengea uwezo kwa watendaji na wafugaji wa samaki.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
KITUO CHA KUZALISHIA VIFARANGA VYA SAMAKI KUZINDULIWA APRILI 20 KITUO CHA KUZALISHIA VIFARANGA VYA SAMAKI KUZINDULIWA APRILI 20 Reviewed by By News Reporter on 4/17/2018 07:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.