Loading...

MWANASIASA KENNETH MATIBA AMEFARIKI DUNIA

Loading...
Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mwanasiasa huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Ken, kama alivyojulikana nchini Kenya ameaga dunia katika Hospitali moja ya kibinafsi ya Karen, iliyoko Jijini Nairobi.

Ken Matiba ambaye ni maarufu katika siasa za ukombozi wa pili wa kisiasa nchini Kenya, baada ya ile ya Uhuru miaka ya 1950s na 1960s.

Mwanasiasa huyo maarufu ambaye alitatiza pakubwa siasa za Rais wa awamu ya pili nchini humo mzee Daniel Toroitich Arap Moi, alizaliwa Juni Mosi mwaka 1932 - na akafariki Jumapili April 15 ya mwaka huu wa 2018.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MWANASIASA KENNETH MATIBA AMEFARIKI DUNIA MWANASIASA KENNETH MATIBA AMEFARIKI DUNIA Reviewed by By News Reporter on 4/16/2018 10:05:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.