Loading...

MAELFU YA WAUGUZI WANAOGOMA WAFUKUZWA KAZI ZIMBABWE

Loading...
Serikali ya Zimbabwe imetangaza kwamba imewafukuza kazi maelfu ya wauguzi wanaoendelea na mgomo wakidai kulipwa mshahara mzuri.

"Kwa maslahi ya wagonjwa na kuokoa maisha ya watu, serikali imeamua kuwafukuza kazi wauguzi wote wanaoendelea na mgomo, hatua ambayo inachukuliwa papo hapo," alisema makamu rais Constantino Chiwenga katika taarifa Jumanne wiki hii.

Bw Chiwenga amewashtumu wauguzi hao kwamba "walishawishiwa kisiasa".

Wagonjwa hawakuweza kuelekea hospitali kuu wiki hii baada ya mgomo wa wauguzi kuanza. Mgomo huo ulianza wiki kadhaa tu baada ya mgomo wa madaktari.

Makamu rais wa Zimbabwe aliongeza kuwa wauguzi wasio na ajira na wastaafu wanatajiria kuchukua nafasi ya wale waliofukuzwa kazi. Jenerali Chiwenga aliongoza operesheni ya kung'olewa kwa rais Robert Mugabe mnamo mwezi Novembea 2017 wakati jeshi lilipochukua kwa muda mfupi udhibiti wa nchi kabla kuteuliwa kwa rais Emmerson Mnangagwa.

Jenerali Chiwenga amesema anasikitishwa na mgomo wa wauguzi wakati ambapo serikali ilitoa dola milioni 17 ili kuboresha mishahara yao. Chiwenga ameongeza kwamba sasa pesa hizi zitatumika kwa kulipa mishahara ya wauguzi wapya.

Chama cha Wauguzi nchini Zimbabwe kimesema kuwa "kimepokea" taarifa ya Chiwenga lakini kitaendelea na mgomo.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
MAELFU YA WAUGUZI WANAOGOMA WAFUKUZWA KAZI ZIMBABWE MAELFU YA WAUGUZI WANAOGOMA WAFUKUZWA KAZI ZIMBABWE Reviewed by By News Reporter on 4/19/2018 08:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.