Loading...
Amini usiamini, pakiti hizo za majani ya chai yaliotumika, zina manufaa makubwa katika taasisi ya sanaa ya Original T-Bag Designs arts and crafts centre huko Hout Bay, nje kidogo ya mji mkuu wa Cape Town.
Wakati bidhaa nyingine katika kituo hicho zina mvuto hususan kwa watalii wa nje, ni mabegi na pochi zilizotengenezwa kwa pakiti hizo za majani ya chai na Gracious Dube zimepata mvuto mkubwa katika tamasha la kuonyesha mitindo ya mavazi huko Paris.
Ni vigumu kutoshangazwa unapotizama ubunifu huu wa sanaa.
Bidhaa zote zimetengenezwa kwa kutumia pakiti hizo za majani ya chai yaliotumika na huwezi kutambua baada ya kutengenezwa na kupambwa na wasaniii 16 wengi wao wanatoka mji ulio karibu wa Imi Zamo Yethu township.
Na bidhaa hizi zimepata umaarufu mkubwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris na ndio sababu ya kupewa jina la Mkoba wa Paris.
Gracious Dube, ambaye ni mzaliwa wa Zimbabwe anasema bado haamini kwamba mkoba wake unauzwa katika mji mkubwa wa mitindo.
Kwa hivyo mara nyingine unapokunywa chai yako ukumbuke pakiti unayotumia ya majani ya chai ni kipato cha wengine na kimetoa nafasi za ajira lakini pia imekuwa fursa kwa wasaniii kuonyesha ubunifu wao.
Na Neema Joshua.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mitindo punde zinapojiri.

POCHI ZILIZOTENGENEZWA KWA PAKITI ZA MAJANI YA CHAI
Reviewed by By News Reporter
on
4/19/2018 11:12:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: