Loading...

MAJINA YA VIONGOZI HUTUMIKA KAMA MBINU MPYA ZA UTAPELI - KENYA

Loading...
Siku kadhaa kupita aliibuka kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Chacha aliyedaiwa kuwalaghai wabunge 13 wa kike wa Kenya na kuwafanyia utapeli akitumia mbinu ya kutoka nao kimapenzi na baadae kutumia mawasiliano ya waheshimiwa hao kufanya utapeli, na baadae alikamatwa na polisi.

Halijatulia la Chacha, siku ya Alhamisi, chombo kimoja cha habari nchini humo, kiliripoti taarifa ya dada mmoja aliyejulikana kwa jina Centrine Nasimiyu Ting'iting'i anayetokea katika kijiji cha Namwesi, kata ya Sirisia kufanya utapeli wa mtindo huo huo kwa kutumia jina la kiongozi wa serikali Gavana wa Bungoma, David Kiui kwa kujifanya ni kaka yake ila polisi walifanikiwa kumkamata.

Dada huyo alikuwa akiwalaghai watu mbali mbali kwa madai angewatafutia kazi kama watampatia kiasi fulani cha pesa na alidai kuwa kaka yake gavana ndio anayempa uwezo huo wa kuwapa watu kazi na endapo watampatia pesa hizo anamperekea gavana huyo kwa ajili ya kuwapatia fursa ya ajira katika kaunti.

Ndipo waathirika na utapeli huo wakaanza kuripoti vituo vya polisi baada ya kugundua wamefanyiwa utapeli ndipo baadae polisi wakafanikiwa kumtia mbaroni.

Atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapo kamilika. Matukio ya utapeli yamekuwa yakifanyika kasi hasa katika kipindi hiki cha muda mfupi na polisi wanapambana na vitendo hivyo kuhakikisha wananchi wanaishi salama.
Na Hamis Fakhi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MAJINA YA VIONGOZI HUTUMIKA KAMA MBINU MPYA ZA UTAPELI - KENYA MAJINA YA VIONGOZI HUTUMIKA KAMA MBINU MPYA ZA UTAPELI - KENYA Reviewed by By News Reporter on 4/07/2018 08:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.