Loading...
Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Makerere amajikutwa akipata mashaka baada ya kunaswa kwenye picha akijaribu kumnajisi mwanafunzi.
Racheal Njeri ambaye ni Mkenya na mwanafunzi wa chuo hicho, alikuwa umeenda kuchukua matokeo yake ya mtihani ndipo alipokumbana na masaibu hayo.
Mhadhiri huyo aliyejulikana kwa jina la Edward Kisuze alimkamata Njeri na kumfungia kwenye ofisi yake baada ya kumshinda kwa nguvu.
Akiwa katika harakati za kujinasua kutoka mikononi mwa mhadhiri huyo, Njeri alisema kuwa alijaribu kila awezalo na kubahatika kumpiga picha huku naye aking'ang'ania kumvua chupi.
"Niliambiwa niende niangalie majibu ya mtihani wangu katika chumba namba 507, na nilifika huko saa nne asubuhi, nikaambiwa nisubiri hadi saa nane na nusu. Nikarudi tena muda huo nikaambia nisubirie dakika 5 ili waangalie kama majibu yangu yapo tayari.
Muda mchache niliitwa ndani na majibu yalikuwa tayari, nilipokuwa nikipekuwa stakabadhi zangu, mhadhiri huyo alinishika na kufunga mlango huku akiniambia kuwa ananipenda.
Alianza kunivua chupi, sikuwa na la ziada kwa sababu alikuwa amenishinda nguvu, ila niliweza kumpiga picha akifanya kitendo hicho," Njeri alisimulia kwenye barua yake ambayo imeenezwa mitandaoni.
Mhadhiri huyo inasemekana kasimamishwa kazi baada ya madai ya njeri kusambaa kote mitandaoni.
Na Catherine Kisese.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za gossip punde zinapojiri.

MWANAFUNZI WA MAKERERE ASIMULIA JINSI MHADHIRI ALIVYOMFANYIA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Reviewed by By News Reporter
on
4/19/2018 01:04:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: