Loading...

WAJASIRIAMALI PEMBA WAWEKA WAZI MANUFAA YAO WATAKA WANANCHI KUSHAJIHIKA

Loading...
Wajasiriamali wa kikundi cha ushirika cha Tekeleza waliyopo Mavungwa shehia ya mbuzini mkoa wakusini Pemba wamesema, kutokana na hali za kimaisha zilivyo hivi sasa ni kheri kwa akina mama kushiriki katika vikundi mbalimbali vya ushirika kwani manufaa ni makubwa kiasi ambacho hata baadhi ya wanaume wanaweza kupata msaada kutoka kwa wake zao.

Waliyazungumza hayo jana mbele ya waandishi wa habari waliyofika katika ushirika huo kwa lengo la kuwatembelea na kutazama mafanikio na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uwendeshaji wa shughuli zao.

Walisema, kupitia ushirika wa Tekeleza ambao ndio kituo kikuu cha ushirika Mavungwa wamefanikiwa kufungua miradi yao mbalimbali na hivi sasa wanaiendeleza vizuri na hali za kiuchumi zinazidi kuimarika.

Bi Sharifa Khamis ambae ni mwanachama wa kikundi hicho kilichojikita zaidi katika ufugaji na kilimo alisema , kupitia Tekeleza amefanikiwa kupata elimu ya ujasiriamali na kuamua kuifanyia kazi na hadi sasa ameshafungua mradi wa kufuga bata mzinga akishirikiana na wananchi wengine .

” nashuruku tunapata pesa , hali sio kama mwanzo, sasa naweza kujipatia mahitaji muhimu katika maisha , nimeshanunua makabati yangu ya kuwekea nguo na cherahani” alisema mama huyo.

Akielezea mafanikio zaidi aliyayapata amesema jambo kubwa na la msingi mpaka hivi sasa anamudu kuwasomesha watoto wake kwa kuwalipia ada za skuli na huduma nyengine jambo ambalo alisema kwake ni faraja kubwa.

Mwanachama mwengine ambae anaonekana kufurahia uwepo wa kikundi cha Tekeleza Bi Lela Seif Khamis alisema mara tu ulipokuja mradi wa kujifunza mambo mbalimbali ya ujasiriamali katika kikundi hicho aliungana na wenzake kutekeleza majukumu ya kikundi huku akipokea taaluma tofauti zilizokua zikimletea mwanga katika maisha.

Alisema kutokana na upeo wa maarifa waliokua wakipatiwa hivi sasa ameshajiwezesha mwenyewe na hali za kimaisha zinakwenda vizuri tofauti na ilivyokua awali.

” sasa naweza kumlipia mwanangu kila mwaka shilingi 15,000/= za skuli, nimenunua friji nauza juisi, nimejenga banda nauza uji , nilikua sina uwezo wowote kipindi cha nyuma lakini hivi sasa mambo yanakwenda vizuri , mana muda mwengine hata mumewangu huchachiwa na akataka nimuazime chochote na nikampatia ” alisema Lela.

Lela alisema , ukiachilia mbali mafanikio hayo lakini pia hivi sasa anaona ndoa yake ipo salama kwani ikitokea mume amekosa, chakupika hakikosi ndani ya nyumba na akirudi chakula tayari wanakula na mambo yanaendelea kama kawaida.

Kwa upande wake katibu wa kikundi cha Tekeleza Bw: Muhammed Bakar Omar alisema lengo la kikundi chao ni kuondosha utegemezi wa kiamisha kwa wananchi na kila mmoja awe na nyenzo ya kujipatia kipato katika maisha.

Alisema kituo chao cha Tekeleza ni katika mradi wa ASSP ambao umelenga kuwakomboa wananchi kiuchimi na hadi hivi sasa harakati za kuwaelemisha zinaendelea vizuri ikiwamo katika sekta ya kilimo na ufugaji.

” tunawafundisha mbinu bora za kilimo na ufugaji , yoyote atakaekuwa tayari nasi huwa tayari kumwelekeza na kisha anaona matunda yake” alisema katibu huyo.

Katibu alifahamisha kuwa ingawa mafanikio ni mengi katika kikundi hicho kama vile kutoa wanachama wengi ambao wanajitegemea lakini pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa pesa za kumalizia jengo pamoja na kutokuwepo kwa huduma ya umeme ambayo ni muhimu sana kutokana na kazi zao.

Hivyo aaliwataka wadau wa maendeleo na washirika wengine kujitokeza kusaidia katika utatuzi wa changamoto hizo ili yale malengo yaliyokusidiwa yafikiwe kwa wepesi zaidi.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
WAJASIRIAMALI PEMBA WAWEKA WAZI MANUFAA YAO WATAKA WANANCHI KUSHAJIHIKA WAJASIRIAMALI PEMBA WAWEKA WAZI MANUFAA YAO WATAKA WANANCHI KUSHAJIHIKA Reviewed by By News Reporter on 4/19/2018 11:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.