Loading...

MWANAMITINDO MJERUMANI ALIYEAMUA KUJIBADILI NA KUWA MWAFRIKA MWEUSI

Loading...
Mwanamitindo Mjerumani wa kwanza kujibadili rangi ya ngozi yake na kuwa nyeusi, abatizwa na kugewa jina la kiafrika alipowasili nchini Kenya.

Mwaka jana, Martina Big mwenye miaka 29, na nywele za blonde na macho ya blue alianza safari yake ya kujibadili na kuwa Mwafrika mweusi. Hii ilikuja baada ya kutumia milioni zaidi ya milioni 40 kukuza matiti yake na kuwa makubwa, ambapo ilimtengenezea umaarufu ya kuwa mwanamke mwenye matiti makubwa Ulaya. Yenye uzito wa kilo 12.

Katika mahojiano na televisheni kadhaa alisema anatamani ngozi nyeusi na ameamua kujibadili ngozi yake na kuwa mweusi.

Mwezi uliopita alianza safari yake ya Afrika kwa kutembelea nchi ya Kenya na ndipo alipo badili jina baada ya kubatizwa na mchungaji Murage kata ya Nyeri na kuitwa "Malaika Kubwa".

Na baadae aliamua kubadili jina lake la zamani kulitambulisha rasmi jina la Malaika Kubwa kuwa ndio jina lake pendwa.
Na Catherine Kisese.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MWANAMITINDO MJERUMANI ALIYEAMUA KUJIBADILI NA KUWA MWAFRIKA MWEUSI MWANAMITINDO MJERUMANI ALIYEAMUA KUJIBADILI NA KUWA MWAFRIKA MWEUSI Reviewed by By News Reporter on 4/22/2018 05:54:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.