Loading...

MWILI WA MTANZANIA ALIYEUAWA NA MUMEWE UINGEREZA KUWASILI KESHO

Loading...
Mwili wa Mtanzania Leyla Mtumwa aliyeuawa na mumewe nchini Uingereza unatarajiwa kuzikwa mjini hapa keshokutwa.

Kaka wa marehemu, Abdulmalik Mtumwa alisema mwili wa Leyla unatarajiwa kuwasili Arusha kesho usiku au keshokutwa asubuhi.

Leyla ni mtoto wa Hidaya Mtumwa, mwanamke aliyewahi kutungiwa wimbo na mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Pepe Kalle miaka ya 1990.

Mtanzania huyo anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na kifuani na mume wake, Kema Kasambula usiku wa kuamkia Aprili 30, nyumbani kwa wanandoa hao Kirkstall Avenue, Haringey nchini humo.

Mwili huo unaletwa kutokana na michango ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza.

Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Watanzania inayotambuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Joe Warioba aliliambia Mwananchi kwa kifupi kuwa waliuaga mwili wa Lelya jana.
Na Catherine Kisese.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MWILI WA MTANZANIA ALIYEUAWA NA MUMEWE UINGEREZA KUWASILI KESHO MWILI WA MTANZANIA ALIYEUAWA NA MUMEWE UINGEREZA KUWASILI KESHO Reviewed by By News Reporter on 4/22/2018 05:15:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.