Loading...
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii kutoka mkoa wa Kigoma Sunday Linex Mjeda alipofunguka na kusema kuwa asilimia kubwa ya wimbo wa lekadutigite ulitengenezwa na kutayarishwa na yeye, msanii mwenzake kutoka Kigoma mwanadada Mwasiti Almasi amefunguka na kusema kuwa Linex kwa sasa hapaswi kuzungumzia mambo hayo zaidi ya kukaa na kuangalia jinsi gani ya kufanya kitu kikubwa kuliko kile.
Na Neema Joshua.Aache kuongelea vitu vilivyopita, lekadutigite ilishapita nadhani kwa sasa inabidi tuangalie yale yaliyopo tu kama familia lazima kuangalia kitu gani tena kinaweza kutuongezea manufaa lakini sio nani kaandika mistari mingapi, au mistari mingi , maana hiyo ni zaidi ya miaka minne sasa.-Aliongea mwasiti katika XXL ya Clouds FM
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MWASITI AAMUA KUMJIBU LINEX KUHUSU WIMBO WA LEKA DUTIGITE
Reviewed by By News Reporter
on
4/22/2018 02:48:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: