Loading...

INDIA YAPITISHA ADHABU YA KIFO KWA WABAKAJI WATOTO

Loading...
Baada ya tafrani zilizozuka kutokana na kifo cha mtoto wa miaka nane,bunge la India limeamua kupitisha adhabu ya kifo kwa yeyote atakayembaka mtoto mwenye umri chini ya miaka 12.

Uamuzi huo umechukuliwa wakati wa mkutano ulioongozwa na waziri mkuu wa India, Narendra Modi katika mji mkuu wa New Delhi.

Kwa wabakaji wa watoto chini ya miaka 16, adhabu imeongezwa kutoka miaka 10 hadi 20 gerezani.

Kosa hilo linaweza kumfanya mbakaji apewe adhabu ya kifungo cha maisha.

Kumekuwa na maandamano katika miji tofauti nchini India kupinga mauaji ya binti wa miaka anne aliyetekwa,kuteswa,kubakwa na kisha kuuawa na kikundi cha wahindu katika eneo la Kathua.

Mwili wa binti huyo ulikutwa umetelekezwa msituni na kupatikana wiki moja baadae.

Sheria hiyo mpya itaanza kutumika baada ya kusaini wa na rais Ram Nath Kovind..

Kwa sasa adhabu ya juu kabisa kwa mbakaji ni kifungo cha maisha.
Na Neema Joshua.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
INDIA YAPITISHA ADHABU YA KIFO KWA WABAKAJI WATOTO INDIA YAPITISHA ADHABU YA KIFO KWA WABAKAJI WATOTO Reviewed by By News Reporter on 4/22/2018 02:29:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.