Loading...
Katika siku ya furaha kuu kwa Wakristo, kiongozi wa kanisa Katoliki papa Francis katika ujumbe wake wa Jumapili ya Pasaka alitoa wito wa amani katika dunia ambayo imegubikwa na vita na mizozo.
Akianza na nchi anayopenda kutoa wito wa amani na inayokabiliwa na vita vya muda mrefu ya Syria," aliendelea katika eneo lote la mashariki ya kati, rasi ya Korea na sehemu za Afrika zilizoathirika na 'njaa, mizozo isiyokwisha na ugaidi."
Francis aliakisi mtazamo wake katika nguvu ya imani ya msingi ya Ukristo kwamba Yesu aliamka kutoka mautini baada ya kuteswa msalabani , katika ujumbe wake wa kila mwaka wa Pasaka unaojulikana kama "Urbi et Orbi" ama "kwa mji na dunia" unaotolewa katika kibaraza cha kanisa la Mtakatifu Petro Basilica katika uwanja wa kanisa hilo uliojaa watu pomoni.
Kiongozi huyo wa kidini amesema ujumbe wa ufufuo unatoa matumaini katika dunia "inayokabiliwa na matukio mengi ya kutokuwa na sheria na matumizi ya nguvu."
"Unazaa matunda ya matumaini na utu ambako kuna udhalilishaji na kutengwa, njaa na ukosefu wa ajira; kule ambako kuna wahamiaji na wakimbizi, ambao kila mara wanakataliwa na utamaduni wa ubadhirifu katika siku hizi, na wahanga wa biashara ya madawa ya kulevywa , biashara ya kusafirisha watu kwa njia haramu na njia za utumwa wa kisasa, " Papa alisema.
Ametoa wito wa "kumalizwa kwa haraka " mauaji nchini Syria, akisisitiza kwamba misaada ipelekwe haraka kwa wanaoihitaji nchini humo na kutoa wito wa "hali inayokubalika ya kurejea na wale waliokimbia makaazi yao."
Na Mohammed Makame.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za ulimwengu punde zinapojiri.

PAPA FRANCIS ATOA WITO WA AMANI DUNIANI
Reviewed by By News Reporter
on
4/02/2018 03:24:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: