Loading...

RAPA CARDI B AFUNIKA KATIKA SHOO YA COACHELLA

Loading...
MWANAMUZIKI wa hip hop wa Marekani, rapa Cardi B, Jumapili ameonesha kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wake katika sherehe  za Coachella zilizofanyika Ukumbi wa Empire Polo uliopo jijini Califonia, Marekani.

Cardi B ambaye ni mjamzito, alipanda jukwaani kuonesha uwezo wake wa kutoa burudani ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki, Beyonce apande kuungana tena na kundi la Destiny’s Child.

Gumzo kwa mwanamuziki huyo liliongezeka baada ya kuvaa nguo iliyobuniwa na Alejandro sawa na kundi la  TLC. Nyota huyo pia alitumbuiza pamoja na kundi la YG, G-Eazy, Chnace The Rapper, Kehlani na 21 Savage.
Na Neema Joshua.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
RAPA CARDI B AFUNIKA KATIKA SHOO YA COACHELLA RAPA CARDI B AFUNIKA KATIKA SHOO YA COACHELLA Reviewed by By News Reporter on 4/18/2018 08:34:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.