Loading...
MWANAMUZIKI nyota Ali Kiba anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa dhati, Amina Rikesh ambaye ni raia wa Kenya, anayeishi Mombasa.
Mipango ya harusi inaendelea kuandaliwa vizuri huku mashabiki zao wao wakisubiri kwa hamu sherehe hiyo ya ndoa yao, ikiwa kituo kimoja cha televisheni (cha AZAMTV) pia kimehaidi kuonyesha moja kwa moja matukio ya harusi.
Mtandao mmoja wa nchini Kenya uliweza kubaini kwamba, Kiba amewanunulia wakwe zake watarajiwa nyumba ya kifahari ambayo wanatarajia kuhamia ndani kabla siku ya harusi kufika.
Kwa mujibu wa mtandao huo, ulitaarifu kuwa Kiba aliamua kufanya hivyo ili kuwapa mazingira mazuri wageni watakaohudhuria harusi yao.
Habari za harusi ya Kiba zilithibitishwa na mdogo wake Abdu Kiba akiwa kwenye mahojiano na gazeti moja hapa nchini.
Abdu alisema kuwa wapenzi hao watafanya sherehe ya ndoa yao kwenye ukumbi mmoja mtaani Kongowea eneo la bunge la Nyali, Alhamisi Aprili 19.
Na Neema Joshua.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

ALI KIBA AWANUNULIA JUMBA LA KIFAHARI WAKWE ZAKE
Reviewed by By News Reporter
on
4/18/2018 09:33:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: