Loading...

WEMA AMTAMANI MTOTO WA MWANAMITINDO HAPPINESS MAGESE

Loading...
MWIGIZAJI mahiri nchini, Wema Sepetu, ameweka hisia zake za kutamani kuishi na Kairo, ambaye ni mtoto wa Happiness Magese, aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2001.

Wema alionyesha hisia hizo kupitia moja ya ukurasa wa kijamii wa Magese, baada ya dakika chache kutupia picha ya mtoto wake.

“Da Happy ukija si utanigaia huyu apa hata siku tatu, naomba tafadhali, ila sijui maana huyu ni zaidi ya roho kwako, aaah mimi nitakuja kukaa na wewe tu hata wiki ili nimng’ate ng’ate mashavu,” aliandika Wema.

Baada ya ujumbe huo, Magese aliibuka na kumjibu Wema kwa kumsihi asikate tamaa badala yake awe na subira kwani siku moja Mungu atamfanyia maajabu na yeye aitwe mama.
Na Peter Godwin.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
WEMA AMTAMANI MTOTO WA MWANAMITINDO HAPPINESS MAGESE WEMA AMTAMANI MTOTO WA MWANAMITINDO HAPPINESS MAGESE Reviewed by By News Reporter on 4/18/2018 10:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.