Loading...

RICK ROSS KUFUNGA BARABARA KUU NAIROBI SHOO YA APRIL 28

Loading...
Rapa maarufu kutoka Marekani, Rick Ross anatarajiwa kufanya shoo wiki ijayo jijini Nairobi - Kenya ambapo atawatumbuiza mashabiki zake katika ukumbi wa Carnivore Aprili 28.

Kulingana na matarajio wa wingi wa watu kuhudhuria katika shoo hiyo waandaaji wa shoo, NGR Redio waliamua kuandika barua kwa gavana Sonko kumuomba kufungwa kwa barabara kuu za Mombasa na Lang'ata kufungwa kuanzia Aprili 27 hadi Aprili 29 ili kurahisisha usafiri wa magari.

Hata hivyo bado haijatamkwa rasmi kama ombi hilo limekubaliwa au la, kwa mujibu wa mtandao mmoja wa habari huko Nairobi.

Rick Ross alisema anahamu ya kufika nchini humo ili asikie ladha ya muziki wa hip hop nchini humo.

Rapa huyo amewahi kushirikiana ma mwanamuziki Diamond Platinumz kutoa wimbo mmoja ambao umefanya vizuri hapa nchini na Marekani unaokwenda kwa jina la 'WAKA WAKA'.
Na Fatma Pembe.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
RICK ROSS KUFUNGA BARABARA KUU NAIROBI SHOO YA APRIL 28 RICK ROSS KUFUNGA BARABARA KUU NAIROBI SHOO YA APRIL 28 Reviewed by By News Reporter on 4/18/2018 10:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.