Loading...

TAARIFA KWA UMMA: MVUA KUBWA ZINATARAJIWA KUNYESHA NCHINI

Loading...
Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku mpaka Aprili 16 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya jana (Ijumaa) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha, TMA imewashauri wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
TAARIFA KWA UMMA: MVUA KUBWA ZINATARAJIWA KUNYESHA NCHINI TAARIFA KWA UMMA: MVUA KUBWA ZINATARAJIWA KUNYESHA NCHINI Reviewed by By News Reporter on 4/14/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.