Loading...
Kulingana na utafiti uliofanywa na 'ReDo', kwa ushirikiano wa Ubelgiji na 'Global Cures' ya Marekani inayopambana na ugonjwa wa kansa, vidonge vya Viagra huweza kutibu saratani ya matiti, ngozi na ubongo.
Mzee mwenye umri wa miaka 80 aliyekuwa akitumia vidonge hivyo kuongeza nguvu za kiume alianza kuonyesha dalili ya kupona kutokana na maradhi yake ya saratani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika hilo Aprili 11.
Aidha ripoti hiyo imebaini kuwa vijana wanne kwenye kliniki moja waliokuwa wakitumia vidonge hivyo walionyesha ishara ya kupona saratani.
Imebainika kuwa PDE5, kemikali inayopatikana ndani ya vidonge vya Viagra ndivyo hutibu kansa.
Licha ya viagra kujulikana kama tembe kuamsha hamu ya tendo la ndoa, imebainika pia kuwa hutibu maradhi ya moyo.
"Hatua zilizopigwa katika matumizi ya 'Sildenafil' maarufu kama Viagra ni ya kuvutia mno.
Mwanzo ilikuwa tiba ya ugonjwa wa moyo kisha ikawa ya kuamsha hamu ya mapenzi na sasa ni tiba ya kansa," Dkt Pan alinukuliwa akisema.
Na Catherine Kisese.
Tuma neno 'AFYA' kwenda +255765112259 kupata habari za afya punde zinapojiri.
TAFITI ZINAONYESHA VIDONGE VYA 'VIAGRA' KUTIBU UGONJWA SARATANI
Reviewed by By News Reporter
on
4/20/2018 09:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: