Loading...
Wakati Mzazi mwenzie akiendelea kukabaliana na misukosuko mbalimbali, Zarina Hassan ametua kwa mara ya pili nchini kimyakimya.
Zari ametua leo mchana akitokea nchini Afrika Kusini yalipo makazi yake akisema amekuja kupiga picha za bidhaa za nepi za watoto aina ya SoftCare, zinazotengenezwa na kiwanda cha Kedz Tanzania.
Mama huyo wa watoto watano na mjasiriamali maarufu, alitangazwa rasmi kuwa balozi kwa miaka mitatu wa bidhaa hizo Machi 28 mwaka huu.
Meneja masoko wa Kedz, Briton Mkocha ambaye ndiye alifika kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), aliiambia Mwananchi kuwa moja ya shughuli zilizomleta kufanya Zari ni pamoja na kupiga picha za video zitakazotumika kwa tangazo la bidhaa hiyo.
Kwa upande wake Zari amesema anajisikia furaha kufanya kazi kampuni hiyo na kueleza kuwa kuna wanawake wengi na warembo hapa Tanzania huenda wangeamua kufanya nao kazi, lakini wameamua kumchagua yeye jambo ambalo ni heshima kwake.
Na Neema Joshua.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

ZARI ATINGA DAR KIMYA KIMYA
Reviewed by By News Reporter
on
4/20/2018 09:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: